Ads 468x60px

Recommended Post Slide Out For Blogger

Wednesday, January 8, 2014

MEZ B - AJERUIWA USONI KWA KISU NA MTU ASIYEJULIKANA


Msanii Mez B, akakatwa katwa na kisu, na kijana asiefahamika, mida ya saa sita za usiku wa kuamkia jumamosi, maeneo ya Carribean, sinza, alipokuwa akisubiri usafiri, akielekea nyumbani kwake.
akiongea nami asubuhi ya leo Maze B. amesema

"nilikuwa natoka kuonana na Noorah, na baada ya kuonana nae, nilipitia sehem inayoitwa Carrebean iliyoko maeneo ya Sinza kwa ajili ya kupata msosi, baada ya kula nikaona nipate na kinywaji kidogo, wakati naendelea na kinywaji  ndipo alikuja jamaa simjui na kuanza kunitukana, nilimshangaa lakini niliachana nae, baada ya muda nikamuona anaongea na mabaunsa, lakini sikufatilia ni nini walichokuwa wakikiongea, baada ya kumaliza kinywaji changu, nilishuka chini maana sehem hiyo  ni ghorofani, wakati nikiwa chini nikisubiri usafiri, ghafla nikamuona yule baunsa amenifata akiwa na yule kijana na kunipeleka pembeni akidai anataka kujua kwanini yule kijana alikuwa akinitukana, lakini baada ya kufika pembeni, yule jamaa akatoa kisu, na kuniharibu vibaya usoni, huku yule baunsa akiangali."

Kwa sasa hali yake inaendelea vizuri!

 

Facebook and Twitter

Promo Sites