Ads 468x60px

Wednesday, January 8, 2014

MEZ B - AJERUIWA USONI KWA KISU NA MTU ASIYEJULIKANA


Msanii Mez B, akakatwa katwa na kisu, na kijana asiefahamika, mida ya saa sita za usiku wa kuamkia jumamosi, maeneo ya Carribean, sinza, alipokuwa akisubiri usafiri, akielekea nyumbani kwake.
akiongea nami asubuhi ya leo Maze B. amesema

"nilikuwa natoka kuonana na Noorah, na baada ya kuonana nae, nilipitia sehem inayoitwa Carrebean iliyoko maeneo ya Sinza kwa ajili ya kupata msosi, baada ya kula nikaona nipate na kinywaji kidogo, wakati naendelea na kinywaji  ndipo alikuja jamaa simjui na kuanza kunitukana, nilimshangaa lakini niliachana nae, baada ya muda nikamuona anaongea na mabaunsa, lakini sikufatilia ni nini walichokuwa wakikiongea, baada ya kumaliza kinywaji changu, nilishuka chini maana sehem hiyo  ni ghorofani, wakati nikiwa chini nikisubiri usafiri, ghafla nikamuona yule baunsa amenifata akiwa na yule kijana na kunipeleka pembeni akidai anataka kujua kwanini yule kijana alikuwa akinitukana, lakini baada ya kufika pembeni, yule jamaa akatoa kisu, na kuniharibu vibaya usoni, huku yule baunsa akiangali."

Kwa sasa hali yake inaendelea vizuri!

Sunday, January 5, 2014

KUMBE CHANZO CHA DIAMOND NA PENNY KUACHANA SIO WEMA...NI KIGOGO MMOJA WA CCM NDIYE ANAHUSIKA

Hata hivyo habri zaidi zinasema kabla ya Bifu hilo halijatokea Diamondi alikuwa
amesha mpatia kiasi cha fedha Penny kwa ajili kutafuta nyumba akapange ili
waishi tofauti na familia jambo ambalo Diamond aligomea kipindi alipokuwa
akiishi na Wema.
"Kwa hiyo Diamond alipoondoka tu kwenda Zanzibar, Penny naye akahama
nyumbani kwao akawa anaishi kwenye hotel moja Sinza, wakati mwingine
alikuwa akionekana hotelini hapo na wifi yake, kipindi hicho ndipo kigogo wa
CCM naye akajitanua zaidi na kuanza kumuhudumia Penny kama mkewe.
"Licha ya kwamba mama na dada wa Diamond walikuwa wakimkubali sana
Penny na kujaribu kumsihi kutomwacha kijana wao lakini Penny alishakuwa
ameonyesha Dalili zote za kutoishio nyumbani kwa mama Naseeb"
Kipindi Fulani Diamond alijaribu kubembeleza uchumba kwa Penny hadi
akauchimba ukoo wao na kugundua kuwa baba yake Penny na Bibi yake
Diamond wamewahi kuishi kijiji kimoja (huko kigoma) hivyo Diamind akazusha
habari kuwa wao ni Ndugu akiamini itamsaidia kuwafanya wazazi wa Penny
anafaa kumuoa binti yao lakini ugunduzi huo ukageuka kuwa kashfa mpya!"
kilisema chanzo hicho
Imebainika kuwa kuvunjika kwa uchumba baina ya Naseeb Abdull 'Diamond'
na Penieli Mwigila kumechangiwa na kigogo mmoja wa CCM ambaye amekuwa
na mahusiano ya kimapenzi na Penny! Swahilitz inakupa full details
Habari za ndani kutoka vyanzo vyetu zimebainisha kuwa tangu siku nyingi
kigogo huyo wa CCM (jina tunalo) amekuwa akilifaidi penzi la mwanadada
Penny kwakuwa anamkono wa birika (mgumu kwenye fedha) licha ya kwamba
fedha anazo.
Akitoboa siri za ndani, mnyetishaji wetu amesema kwamba mbali ya ubahili wa
Diamond pia ndugu wa upande wa Penny hawakuwa wakipenda binti yao aishi
na Diamond kwa kuwa hana sifa za kuishi naye hali iliyo mrahisishia kigogo
huyo kula vya watu



"Amini kwamba katika kipindi chote cha mahusiano yao, Diamond hajawahi
kusalimiana na mama yake Penny hata siku moja, hata kaka zake Penny
hawataki kabisa kumsikia Diamond na mara kibao wamekuwa wakimsema sana
Penny kuhusu Diamond" kimesema chanzo chetu
Kikaongeza "Hata kuachana kwao ni Penny ndiye aliyemuacha Diamond kwa
sababu ambazo si za msingi sana kwani siku nyingi Penny alishakata tamaa ya
kuishi na Diamond
"Nakumbuka kipindi baba yake Wema alipofarikil, Diamond alitaka kwenda
msibani kuzika lakini alikuwa anashindwa atamuagaje Penny, hivyo akaamua
amsukumizie mzigo Babu Tale ili ampigie simu na kujifanya yeye ndiye
aliyemshinikiza kwenda kuzika"
"Sasa siku Diamond alipoaga kwenda Msibani, Penny 'akamtaiti' na kumuuliza
anakwenda kumzika nani? Diamond akamwambia amuulize Babu Tale lakini
Penny alimgomea na kumwambia wewe ndiye unayekwenda kuzika na wewe
ndiye unayenihusu nitamuuliza vipi Babu Tale?
"Diamond akawa hana cha kujibu zaidi ya kuzuga kisha baadae kuondoka na
kwenda Zanzibar kuzika" kilisema chanzo hicho








 

Facebook and Twitter

Promo Sites