Ads 468x60px

Wednesday, September 12, 2012

CHRIS BROWN AKANUSHA UWEPO WA SURA YA RIHANNA KWENYE TATOO YAKE MPYA.

Mkali wa miondoko ya Rnb and Pop nchini marekani Chris Brown a.k.a Brizzy amekanusha vikali kuhusishwa na uwepo wa Sura ya mwanadada Rihanna katika Tatoo yake mpya aliyoichora hivi karibuni. baada ya vyombo vya habari mbalimbali kusambaza habari ya kwamba tatoo ya mkali huyo ina sura ya Rihanna, Chris amekanusha na kusema Tatoo hiyo si Sura ya Rihanna na badala yake ni alama yenye sura ya Mwanamke ambayo chimbuko lake ni Mexico. Tatoo hiyo inaonyesha Fuvu la mwanamke na upande mwingine sura iliyokamilika. Ni ishara inayosherehekewa nchini Mexico kukumbuka vifo..

Lakini ukizitazama kwa karibu utaona zinafanana na Rihanna kwa kiasi kikubwa sana. Kuanzia Macho, Midomo, juu ya Mdomo na alama kwenye Uso zinazoelezea mtindo maharufu wa Nywele uitwao Rihanna.



SOURCE: TMZ

NEW JOINT: GNako ft. Nikki wa 2- Bado Ngware

GNako ft Nikki wa 2- BAdo Ngware




Tuesday, September 11, 2012

MISSY ELLIOT IS BACK!!!!!!


Missy Elliott

Imekuwa kimya kirefu sana toka mkali wa miondoko ya hip hop na Rnb, Missy Elliott alipoachia album yake na single zake za mwisho, 2005.

Hivi karibuni mkali huyo amesikika akisema kuwa ameingia studio na Producer machachali mwenye beats za kumtoa nyoka pangoni, Timberland a.k.a Timbo na kufanya hits mbili kwa jina la "9th Inning" na "Triple Threat"

Single hizi zilizo pair anatarajia kuaziachia mnamo mwezi huu wa September. Tukae mkao wa kula kwa kazi hizi machachali. Dah hakuna kama Mssy kwenye flows na beats za ajabu..

We Miss you Miss Elliott....

LIL WAYNE AMSHTAKI QUINCY JONES III

LIL WAYNE

Lil wayne na Team yake ya Young Money Cash Money Brothers (YMCMB) wamemchukulia hatua za kisheria Quincy Jones kwa kutumia baadhi ya nyimbo zake katika Documentary ya Mkali huyo aliyoipa jina la "THE CARTER".
QUINCY JONES III

Ndani ya Documnetary hiho zimesikika baadhi ya nyimbo za Lil Wayne ambazo zinapatikana katika album ya Carter III iliyompa mauzo makubwa sana Lil Wayne . baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na "Let the Beat Build," "Lollipop,"
na  "Mr. Carter" and "A Milli".

Lil Wayne amekanusha na kusema kwamba Producers wa documentary hiyo hawakuomba kibali wala ruhusa yoyote kwake dhidi ya matumizi ya Nyimbo za mkali huyo.
SOURCE: http://www.prefixmag.com/news/lil-wayne-sues-quincy-jones-son-over-unauthorized-/68813/
 

Facebook and Twitter

Promo Sites