Ads 468x60px

Recommended Post Slide Out For Blogger

Wednesday, September 12, 2012

CHRIS BROWN AKANUSHA UWEPO WA SURA YA RIHANNA KWENYE TATOO YAKE MPYA.

Mkali wa miondoko ya Rnb and Pop nchini marekani Chris Brown a.k.a Brizzy amekanusha vikali kuhusishwa na uwepo wa Sura ya mwanadada Rihanna katika Tatoo yake mpya aliyoichora hivi karibuni. baada ya vyombo vya habari mbalimbali kusambaza habari ya kwamba tatoo ya mkali huyo ina sura ya Rihanna, Chris amekanusha na kusema Tatoo hiyo si Sura ya Rihanna na badala yake ni alama yenye sura ya Mwanamke ambayo chimbuko lake ni Mexico. Tatoo hiyo inaonyesha Fuvu la mwanamke na upande mwingine sura iliyokamilika. Ni ishara inayosherehekewa nchini Mexico kukumbuka vifo..

Lakini ukizitazama kwa karibu utaona zinafanana na Rihanna kwa kiasi kikubwa sana. Kuanzia Macho, Midomo, juu ya Mdomo na alama kwenye Uso zinazoelezea mtindo maharufu wa Nywele uitwao Rihanna.



SOURCE: TMZ
 

Facebook and Twitter

Promo Sites