Ads 468x60px

Recommended Post Slide Out For Blogger

Wednesday, January 15, 2014

MCHOMVU, B12 & DIVA ''OUT OF CLOUDS''




WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es
Salaam, Hamisi Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi
‘Diva’, wamepigwa chini na kituo hicho, Risasi Mchanganyiko
linakupa zaidi.
Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa,
uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na
tabia ya utovu wa nidhamu kwa watangazaji hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba, watangazaji hao
wamesimamishwa kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho
ya Miaka 14 ya Clouds FM, yaliyofanyikia hivi karibuni katika
Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya, Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Muhatahaba na kumwuliza
juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.
“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na
Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na
ofisi, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu
kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana, ingawa watu wengi
wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni
kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza
watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila
kufafanua zaidi.
Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema:
“Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa
hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usijulikana
wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba
wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”
 

Facebook and Twitter

Promo Sites