Ads 468x60px

Recommended Post Slide Out For Blogger

Saturday, December 21, 2013

KIDOTI FASHION CLUB

Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti
brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate
Mwegelo aimeanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti
Club.
Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana, Jokate alisema
kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio
wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali
katika jamii husani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia
alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa
kidoti Brand.
Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri
mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki,
filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika
tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao
wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye.
Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili
mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa
kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata
taarifa mbalimbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo
kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.
“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa
jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu
anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu
yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu
mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema
Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi.
Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbalimbali kwa
wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.
“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji
chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu
name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea
mtu yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu
katika kukabiliana na masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.

 

Facebook and Twitter

Promo Sites