Ads 468x60px

Recommended Post Slide Out For Blogger

Tuesday, April 16, 2013

MADEE KUTOA VERSION MBILI ZA "POMBE YANGU" NA DVD KWA MASHABIKI SIKU YA UZINDUZI



Mwezi huu wa nne ndio mwezi ambao madee amepata mafanikio kwa mara nyingine tena, baada ya kuachia ngoma inayofanya vizuri sana kwenye chati mbali mbali na kwenye maskio na midomo ya watu wengi, hata kufikia kuingia katika nafasi ya kwanza kwenye best chat show bongo "top 20" ya Clouds Fm. Lakini pia ni mwezi ambao amezaliwa yeye, na kufikisha miaka yake kadhaa siku ya tarehe 23, na tarehe 21 anatarajia kufanya uzinduzi wa video ya wimbo wake "pombe yangu" ndani ya maisha club, akizungumza na blog hii, Madee amesema, anatarajia kuachia video mbili za wimbo huo, moja ikiwa ni ya kiasili na nyingine ya kimjini mjini. Licha ya kuachia video hizo, Madee pia atatoa dvd kwa mashabiki kwenda kuzitazama ka muda wao kutokana na kuelewa matatizo yanayotokana na kuhamia kwenye digitali. kwenye show ya uzinduzi huo, atakuwepo pia , Bibi cheka, Diamond pamoja na Tunda man.
 

Facebook and Twitter

Promo Sites