

Mkali wa Hip Hop kutoka nchini Marekani ambaye hivi karibuni
aliitikisa Bongo pale alipopanda jukwaani wakati wa kilele cha Fiesta
mwaka huu, Rick Ross,yupo matatani baada ya kushtakiwa na wadhamini wa
show aliyofanya hivi karibuni huko Miami.
Ilikuwaje?Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali ikiwemo
AllHipHop,kampuni
ya SM Global Union ilikuwa imeingia mkataba na Rick Ross (Rozay) kwamba
atapiga show isiyopungua lisaa lizima.Ilikuwa alipwe $90,000. Tofauti
au kinyume na mkataba huo,Rick Ross, alikuwepo jukwaani kwa jumla ya
dakika 15 tu. Kufuatia kitendo hicho,waandaji hao wameamua kumburuza
Rick Ross mahakamani na kudai jumla ya $226,000 kama fidia.