Ads 468x60px

Wednesday, December 25, 2013

GUPSY`s DELIGHT NOW OPEN IN LAGOS

Aliyekua mwakilishi wa shindano Big Brother Africa msimu wa 4 (Revolution) Elizabhet Gupta ma mumewe  Kevin Chuwang Pam (mshindi wa BBA4) wamefungua mgahawa wao nchini Nigeria.

Mgahawa uitwao Gupys Delight upo jijini Lagos nchini Nigeria ambako ni makazi ya wanando Liz na Pam. Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Liz ameonesha picha za mgahawa huo.


Mwonekano wa mgahawa huo kwa ndani!



Kwa sasa mastaa hao wana familia ya watoto wawili.
All the best Liz and Pam

Tuesday, December 24, 2013

NILIPATA UJAUZITO NIKIWA NA UMRI MDOGO SANA - MADAMNRITA


Kuelekea mwishoni mwa mwaka huwa kila mtu ana utaratibu wake wa kumaliza mwaka.Hivi ndivyo Madam Rita kutoka kampuni ya Benchmark Production ameamua kuufunga mwaka huu.


Madam Rita kupitia akaunti yake ya Facebook amekuwa akitoa stori mbalimbali zinazomuhusu juu ya mambo mengi ambayo yamewahi kumtokea/ kumpata kipindi cha nyuma au katika maisha yake kiujumla.
Moja ya vitu hivyo ni suala ya yeye kupata mimba katika umri mdogo ambalo ameamua kuliweka wazi kwenye ukurasa wake wa FB kama hivi…

Huu ndio ujumbe wake alioupost ' 

Jambo mmoja msilofahamu kuhusu mimi.... 
Nilipata ujauzito nikiwa na umri mdogo sana. Kwa jamii yetu inayotuzunguka, ukizaa katika umri mdogo, watu huwa wanakunyanyapaa, hukuona haufai kuwa katika jamii na hata kukuhukumu. Kwa umri ule niliona ni kama hamna tena maisha kwangu lakini sikukata tamaa na leo hii ujasiri wangu na kitu kinachonipa msukumo wa maisha hadi kufika hapa nilipo ni hicho kilichonikuta nikiwa na umri mdogo.
"Kukataa tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza'Aliandika Madam Rita.

 

Facebook and Twitter

Promo Sites